MWIMBAJI maarufu wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando pichani na mwenzake Enock Jonas (Zunguka) wanatarajiwa kutia chachandu katika tamasha la kwanza kubwa kufanyika Mkoani Kagera.Tamasha hilo la Shangwe Kagera lina lengo la kuielimisha jamii na kuamsha mwamko wa kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika maisha magumu. Mkurugenzi wa Kampuni ya Beula Communications Ltd, ambao ni waandaji wa tamasha hilo, Melkizedeck Mutta, anasema kuwa matayarisho ya tamasha hilo yanaendelea vizuri kutokana na mwitikio mkubwa wa watu mbalimbali waliojitokeza kushiriki.
Pia, Mutta alisema bendi ya muziki
ya wazawa mkoa huo, Kakau Band pamoja na vikundi vingine vya wanakwaya wa makanisa mbalimbali, kikundi cha watoto
yatima wanatarajia pia kutumbuiza. Mutta anasema tamasha hilo la aina yake linatarajiwa kufanyika Uwanja wa Kaitaba na pia kwenye ukumbi wa
Lina’s mjini Bukoba, siku ya Uhuru, Desemba 9.
“Mpaka sasa tumekamilisha sehemu
kubwa ya matayarisho hayo ikiwamo kulipia
uwanja pamoja sehemu ya malipo kwa wasanii ambao watashiriki,”
alisema.
Pia, mkurugenzi huyo aliwaomba
wadhamini zaidi na wadau wengine wa maendeleo ya watoto kujitokeza kushiriki ili
kuwasaidia jamii hasa watoto yatima na wengine wanaoishi katika mazingira
magumu. Muta alisema malengo ya tamasha hilo ni kuhamasisha jamii kuishi kwa
amani, kupendana na kusaidia watu wengine hasa wasiojiweza kimaisha ili na wao wajione ni sehemu
yao.
Katika kutambua hilo kampuni yetu iliamua kufanya
utafiti mdogo nakugundua changamoto nyingi katika Mkoa wa Kagera, mojawapo ni
kuwa na watoto wengi wanaoishi katika
mazingira magumu. Baada ya kuliona hili, tulitembelea vituo mbalimbali vya
kulelea watoto hao, mojawapo ni Tumaini Children’s Centre kinachomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Ki
lutheri Tanzania (KKKT).
Kituo hiki kinalea watoto wote
bila kujali kabila,jinsia wala dini zao,
kwa sasa kituo hiki kinahudumia watoto zaidi ya 800, kwa kuwapatia
elimu,chakula, malazi n.k ambapo kwa
muda mrefu kimekuwa kikipata msaada toka Sweden ambao kwa sasa wametangaza
kuusitisha kwa maelezo kuwa jamii ya Watanzania inapaswa kujifunza na kuanza
kuhudumia watu wao wenyewe.
Kutokana na hilo ndiyo maana
tumeonelea tuwe na tamasha la kuamasisha jamii ili ianze kuona umuhimu wa
kusaidia wenzao wanaohitaji
msaada.
No comments:
Post a Comment