ROSE MUHANDO HR BANNER

ROSE MUHANDO HR BANNER

ROSE MUHANDO SONG OF THE WEEK

Friday, April 12, 2013

MKOA WA IRINGA WATIKISWA KATIKA PASAKA 2013 NA UIMBAJI WA ROSE MUHANDO

Rose Muhando alikuwa gumzo mjini Iringa kwa uimbaji wake. Mkoa wa Iringa ulifurahishwa na huduma ya mwimbaji huyu. Watu walifurika uwanjani mapema kuangalia kitimutimu cha waimbaji wa nyimbo za injili akiwemo Malkia wa Muziki wa Injili Tanzania Rose Muhando.

Rose Muhando

rose mhando na jeshi lake akiwasalimia wana iringa kabla ya kuanza kazi

kazi imeanza vilipigwa viduku vya yesu vya maana




SOLOMONI MKUBWA AKIFANYA AKIMWIMBIA MUNGU

Solomon mukubwa kutoka nchni kenya akiwajibika jukwaani katika uwanja wa samora mkoani iringa




umati mkubwa wa wapenzi wa mziki wa injili wakishuhudia waimbaji hao









kila aliyekua na kitambaa ama kushika kitu chochote mkononi alitakiwa kukinyanyua juu
cloud ya wapenzi wa mziki wa bwana


waimbaji mbalimbali walihudhuria tamasha hilo mbali ya rse mhando na solomon mukubwa pia alikuwepo bonny mwaitege, upendo nkono na wengine wengi wa mikoa ya nyanda za juu kusini.

HABARI ZA ROSE MUHANDO KUTOKA KATIKA BLOGS KUHUSU PASAKA 2013

Na Mwandishi Wetu

MWIMBAJI mahiri wa muziki wa kiroho nchini, Rose Muhando ameongoza kwa kupata kura nyingi kwa mashabiki wanaotaka atumbuize kwenye Tamasha la Pasaka mwaka huu.


Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo,Alex Msama ilieleza kuwa msanii huyo amepata asilimia kubwa ya mashabiki wanaotaka atumbuize kwa waimbaji wa ndani, hivyo tayari kamati yake imempitisha kushiriki tamasha hilo.

“Tunaendesha kura ya maoni kwa mashabiki wetu kwa njia ya kutuma ujumbe mfupi wa maandishi au kupiga simu kuelezea ni waimbaji gani wa ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania wanaotaka wawepo kwenye tamasha la mwaka huu.

“Kwa hiyo mwimbaji Rose Muhando amepata asilimia kubwa ya mashabiki wanaotaka awepo, zaidi ya asilimia 90 wanamtaka Muhando. Hivyo huyo tayari anakuwa tumeshampitisha tunaomba mashabiki waendelee kutuma maoni yao kwa kamati yangu ili kupitisha wasanii wengine.

“Dhamira ya tamasha letu mwaka huu ni liwe la aina yake na tuwashirikishe mashabiki wetu, ndiyo sababu kuanzia mikoa litakapofanyika mpaka suala la waimbaji tumewapa fursa mashabiki wenyewe wateue,” alisema Msama na kuongeza kuwa msanii atakeyekuwa amepigiwa kura kwa wingi ndiye watakayemtangaza.

Tamasha la Pasaka limepangwa kufanyika Machi 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

Source: http://www.fullshangweblog.com/2013/03/01/rose-muhando-angara-tamasha-la-pasaka/

ROSE MUHANDO ALIPOTIKISA KATIKA TAMASHA LA PASAKA 2013 NYUMBANI KWAKE DODOMA

Rose kama ilivyo kawaida yake anapokuwa katika jukwaa, huwa haaichi watu wa Mungu wakiboreka. Rose Muhando siku hii aliwashangaza watu kwa uimbaji wake na kucheza kwake. Rose Muhando kila umuonapo ni mtu wa kutabasamu na kucheka hata anapokuwa jukwani au madhabahuni. Ngoja nikupe kiduchu cha Dodoma

Maliki Rose Muhando.

Vijana wa Dar a.k.a wazee wa mwendo Glorious worship team.


Sauti ya Asali Upendo Kilahiro

Anastazia mkabwa kutoka Kenya.



Dada yangu wa karibu Upendo Nkone akifanya kweli

Boni Mwaitege na "mama ni mama"

Solomoni Mkubwa

Mkurugenzi wa Tamasha la Msama Promotions Ltd Bwana Alex Msama akisalimiana na mgeni rasmi wa tamasha hilo,naibu spika wa bunge Mh.Job Ndugai.


Monday, April 1, 2013

ROSE MUHANDO ALIVYOTIKISA TAMASHA LA PASAKA 2013 JIJINI DAR ES SALAAM

Pamoja na Mvua Kubwa iliyonyesha leo katika jiji la Dar-es-Salaam Maelfu Ya Wakazi wa Jiji la Dar wamejitokeza katika Tamasha la Pasaka lililofanyika katika Uwanja wa Taifa.

Tamasha Pasaka ni Tamasha linalofanyika Kila Mwaka mara moja katika Msimu wa Pasaka ambapo wanamuziki wa nje na ndani ya Tanzania wanakuwa na muda wa pamoja wa Kusifu na Kumwabudu Mungu.

Mwaka 2013 Kauli Mbiu ya Tamasha ni Amani na Utulivu ambapo fedha zitakazopatikana ni maalum kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Katika siku ya leo Mgeni rasmi alikuwa ni Mhe. Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye mara kadhaa alipata shuruba ya kupigiwa makelele mara kwa mara kutokana na kukatika katika kwa umeme mara kwa mara.

Mwanamuzi Mwalikwa wa Mwaka huu Kutoka Africa ya Kusini ni Sipho Makabane ambaye jioni ya leo amefanya Performance ya nyimbo 10 Mfululizo ndani ya uwanja huo na Kukonga nyoyo za watu waliohudhuria Tamasha la leo. Malkia wa Muziki wa Injili Tanzania Rose Muhando alifanya kile ambacho kilitarajiwa na Wakazi wa Jiji kwa Kuimba wimbo wa Utamu wa Yesu ulioombwa na Mhe. Mgeni rasmi.

Wanamuziki Wengine waliokuwepo siku ya leo ni Christ Ambassadors kutoka Rwanda, Solomon Mukubwa, Anastazia Mukabwa, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, John Lisu, Faraja Mtabobwa na Glorious Worship Team.

Malkia wa Muziki wa Injili Rose Muhando akiwa Kikazi Zaidi
Team.

Mwanamuziki Wa Injili wa Tanzania Upendo Kilahiro akienda sawa Siku Ya Leo


Upendo Nkone akiwa Jukwaaani
Sawa siku Ya Leo


Waimbaji Wa Christ Ambassadors kutoka Rwanda walishuka Kutoka Jukwaani na kugusa wanakazi wa jiji la dar na wimbo wao "Kwetu Pazuri"

Anastazia Mukabwa kutoka Kenya akiwa na Rose Muhando ambao kwa pamoja wameimba wimbo wa "Kiatu Kivue"
Christ Ambassadors Choir wakiwa tayari kwa ajili ya Kazi.


Solomoni Mukubwa akiwa anapadna Stejini tayari kwa ajili ya Kuimba siku ya leo


Ephrahim Sekeleti Mwuimbaji Kutoka Zambia akiwa George Mpella na Hudson Kamoga

Glorious Worship Team wakienda Sawa siku Ya Leo

Ephrahim Sekeleti akienda Sawa Siku Ya leo

Sipho Makabane akiwa kikazi Zaidi siku Ya leo

Sehemu Ya Umati Wa Watu


Rose akiendelea na Kazi huku Waandishi na Walinzi wakiwa wamemzunguka

Sipho akijiandaa kuingia Jukwaani

Pole Pole akisogelea Umati Wa watu

Koti Likawa Zito

Kikazi Zaidi

Hapa wakitengeneza Tangazo la Chomoza

Bon Mwaitege akiwa mbele ya Camera Man Ray wa Clouds Tv.

Wakati Sipho akiimba ni kama ilikuwa Mchaka Mchaka Kulia ni Anastazia, Rose Muhando Upendo Nkone na Solomon wakimpa Support Sipho.

John Lisu


Without Caption

HABARI ZILIZOPITA

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...