ROSE MUHANDO HR BANNER

ROSE MUHANDO HR BANNER

ROSE MUHANDO SONG OF THE WEEK

Thursday, November 22, 2012

HABARI ZILIZOTOKA KATIKA BLOG YA LADY JAYDE KATIKA BLOGU YAKE KUHUSU ROSE MUHANDO NA BAHATI BUKUKU - Wednesday, December 16, 2009


BAHATI BUKUKU NA ROSE MUHANDO, WAMEJARIBIWA KUTAPELIWA NA WAHUNI KWA JINA LA BINTI MACHOZI
BAHATI BUKUKU

Watu wasiojulikana mmoja wao akiwa ni mwanamke aliempigia simu mwimbaji wa muziki wa injili Tanzania Bahati Bukuku, alijitambulisha kuwa yeye ni Jide na alikuwa amekwenda safarini Kilombero kurekodi nyimbo za Injili lakini akapata matatizo na kuwa amekwama anahitaji msaada wa haraka sana.

Msaada aliokuwa akiuhitaji huyo Jide feki ni fedha taslimu shilingi za kitanzania Milioni moja
Bahati Bukuku aliamini na akawa tayari kutoa msaada huo kiasi kwamba aliamua kuwatumia kwanza hela ya simu alfu arobaini ambayo walidai wanaihitaji kwa haraka sana ili kuweza kuwasiliana na ndugu wengine wa huyo aliyejiita Jay Dee.
Bahati aliwatumia voucher ya kiasi hicho huku akiwaahidi kujipanga kwanza ili aweze kuwatumia fedha hizo
Lakini MUNGU akamsaidia akakumbuka tu ngoja ampigie Gardner amuulize kama kweli nilikuwa nimepatwa na matatizo hayo.

Alipiga simu akampata Gardner akamuuliza kama anaweza kuongea na mimi ili asikie sauti yangu na aniulize kama nilikuwa nimepatwa na tatizo lolote nahitaji msaada wake.
Nilibakia kushangaa tu na kumuelezea tu kuwa huenda hao wakawa sio watu wazuri.
Ukizingatia sijawahi kuzoeana na Bahati Bukuku hata namba yake ya simu sikuwa nayo wala

 ROSE MUHANDO

Story haikuishia hapo, walipoona Bahati Bukuku anawacheleweshea kukamilisha ma dili yao ndipo walipompigia simu mwanamuziki mwingine maarufu wa Injili Rose Muhando na kumwambia kuwa mume wangu Gardner alikuwa amepata ajali mbaya sana ya gari na ameumia vibaya mno,
kwahiyo nahitaji kiasi cha shilingi milioni mbili ili niweze kutatua matatizo hayo.
Rose aliamua kumpigia promoter wa muziki wa injili Alex Msama na kumuuliza kama ni kweli kuna kitu kama hicho.
ambapo Alex alinipigia simu asubuhi na simu ilipokelewa na Gardner kama kawaida manake mimi sipendi kabisa maswala ya simu, na akashangaa na kuanza kumuelezea yaliotokea.

Gardner alimuambia kuwa siku moja kabla tulipokea simu kutoka kwa Bahati Bukuku akituelezea jaribio kama hilo lilimtokea yeye pia kwa nia ya kumtapeli kutumia jina la Binti Machozi.

Mwisho tu jamani mimi binafsi kama Jay Dee nawaomba watu kuwa makini na haya maswala kwani mji na dunia vimeharibika sana.

Nikipata tatizo kubwa wa kwanza kumuelezea ni Mume wangu na mama yangu mzazi, wao wakishindwa kutatua ndio wataweza kujua nani wa kumwambia.
Na kama hao hawataweza ninao marafiki wengine wengi lakini msiwadanganye wadada wa watu na kuwatia majaribuni bure, Hivi hata mngempigia Ruge basi mumdanganye hayo maswala

Nawasihi sana msidanganyike.

Source: http://ladyjaydee.blogspot.com/2009/12/bahati-bukuku-na-rose-muhando.html

No comments:

Post a Comment

HABARI ZILIZOPITA

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...