
Nilipokaa chini nikaona hakuna sababu ya kuwapoteza hawa vijana na kuliacha kanisa linaanguka. Makanisani kumejaa sana wazee na wale waliovuka ujana, na hii inaashiria kuwa baada ya miaka kadhaa kanisa litaanguka kwani wazee watakuwa wamechoka kufanya kazi ya Mungu.
Vijana wamekuwa wanakimbia kwaya na kuanza kuimba nyimbo za kijamii, na hii inatoka na kukosa watu wa kuwatia moyo na kuonyesha utamu wa kumuimbia Mungu. Hakuna watu wanaoweza kuwahamasisha vijana kufanya kazi ya Mungu. ha hii imesambaaa sana vijijini, vijana wengi vijijini wamemuacha Yesu na kushiriki matendo yasiompendeza Mungu. Kwahiyo nimeona ni vizuri nianzishe semina ambazo zitawafanya vija wafurahie wokovu na wampende Yesu.
No comments:
Post a Comment