ROSE MUHANDO HR BANNER

ROSE MUHANDO HR BANNER

ROSE MUHANDO SONG OF THE WEEK

Thursday, November 15, 2012

MUNGU AMEKUWA MWEMA KUNIWEZESHA KUINGIA STUDIO. WAKO WENGINE WANATAMANI LAKINI WANASHINDWA KUINGIA STUDIO.

Namshukuru Mungu kwa kunipa kibali cha kuingia studio kufanya kazi ya Mungu kwa njia ya uimbaji. Kuna watu wengi wako mitaani na wanatamini kumwimbia Mungu lakini inakuwa ngumu kupata nafasi ya kuweza kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Tatizo kubwa linalowakumba ni kukosa fedha za kulipia studio.

Naomba tutiane moyo, kuwa mwaminifu mbele za Mungu na kufanya yale Mungu anataka ufanye. Kuwa mvumilivu katika kazi unafanya na uwe na malengo makubwa. Nia yako ya uimbaji ichoche ipo siku Mungu atafungua milango na utajishangaa unaingia studio. Mheshimu sana Mungu wako na usipende kutenda dhambi. Mungu hatamani mtu aliyevuguvugu.

No comments:

Post a Comment

HABARI ZILIZOPITA

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...