ROSE MUHANDO HR BANNER

ROSE MUHANDO HR BANNER

ROSE MUHANDO SONG OF THE WEEK

Friday, April 12, 2013

HABARI ZA ROSE MUHANDO KUTOKA KATIKA BLOGS KUHUSU PASAKA 2013

Na Mwandishi Wetu

MWIMBAJI mahiri wa muziki wa kiroho nchini, Rose Muhando ameongoza kwa kupata kura nyingi kwa mashabiki wanaotaka atumbuize kwenye Tamasha la Pasaka mwaka huu.


Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo,Alex Msama ilieleza kuwa msanii huyo amepata asilimia kubwa ya mashabiki wanaotaka atumbuize kwa waimbaji wa ndani, hivyo tayari kamati yake imempitisha kushiriki tamasha hilo.

“Tunaendesha kura ya maoni kwa mashabiki wetu kwa njia ya kutuma ujumbe mfupi wa maandishi au kupiga simu kuelezea ni waimbaji gani wa ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania wanaotaka wawepo kwenye tamasha la mwaka huu.

“Kwa hiyo mwimbaji Rose Muhando amepata asilimia kubwa ya mashabiki wanaotaka awepo, zaidi ya asilimia 90 wanamtaka Muhando. Hivyo huyo tayari anakuwa tumeshampitisha tunaomba mashabiki waendelee kutuma maoni yao kwa kamati yangu ili kupitisha wasanii wengine.

“Dhamira ya tamasha letu mwaka huu ni liwe la aina yake na tuwashirikishe mashabiki wetu, ndiyo sababu kuanzia mikoa litakapofanyika mpaka suala la waimbaji tumewapa fursa mashabiki wenyewe wateue,” alisema Msama na kuongeza kuwa msanii atakeyekuwa amepigiwa kura kwa wingi ndiye watakayemtangaza.

Tamasha la Pasaka limepangwa kufanyika Machi 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

Source: http://www.fullshangweblog.com/2013/03/01/rose-muhando-angara-tamasha-la-pasaka/

1 comment:

  1. Deleon Richards is an American young and sensation gospel singer she became the youngest person ever to be nominated for a Grammy Award the previous record holder was king of pop Michael Jackson. Thanks for sharing your great blog.

    ReplyDelete

HABARI ZILIZOPITA

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...