ROSE MUHANDO HR BANNER

ROSE MUHANDO HR BANNER

ROSE MUHANDO SONG OF THE WEEK

Wednesday, January 23, 2013

JINA LA YESU LINA HERUFI CHACHE LAKINI LINAFANYA MAKUBWA

Leo nimeona nitupie haya maneno niliyoyaimba katika wimbo wangu wa Jina la Yesu, ili na wewe upate kubarikiwa na kuona thamani ya jina la YESU

Rose Muhando

Habari njema kwako kuhusu jina la Yesu,
Raha yangu ni jina la Yesu
Uzima wangu ni jina la Yesu
Habari yangu ni jina la Yesu

Ni jina jema kwa watu wote.
Linasisimua ukilisikia.
Linaleta raha kulitamka.
Linafanya mambo ukiliamini

Jina hilo waliolikataa, lakini kwa wengine limetujengea heshima.

Jina la Yesu ni kwa wgonjwa, ni afya kwao
Jina la Yesu kwa maskini
Jina la Yesu kwa walioachwa
Jina la Yesu kwa walemavu
Jina la Yesu kwa waliosahauliwa ni tumaini Jipya
Jina la Yesu waliolikataa wasomi limetujenge heshima
Jina la Yesu kwa waimbaji
Jina la Yesu kwa yatima
Jina la Yesu ni uzima kwetu
Jina la Yesu lina thamani

Jina nalipenda sana, Jina libarikiwe
Jina liheshimiwe na watu wote, Jina linaokoa

Hatukuwa hivi kama mnavyotuona.
Tulidharauliwa na kukataliwa.
Kwenye jamii yetu tulisahauliwa.
Tulipowauliza swali walitukemea.
Tulipotoa hoja walitudharau.
Lakini Yesu mwenye huruma akayaoona mateso yetu, akatukumbatia.

Kuna mjina mengi duniani lakini hili ni kiboko.
Jamni mimi nimesikia majina mengi, lakini hili la Yesu ni mwanzo mwisho.
Nimesikia majina katika viatbu na doria, lakini hili ni mwanzo mwisho.

Hata kama kwa wengine halifai lakini kwangu limenipandisha juu hili jina la Yesu.
Jina la Yesu lina herufi chache, lakini linafanya mambo makubwa.
Acheni nilipende hili jina la Yesu.

MUNGU AKUBARIKI

Mwandishi
Rulea sanga

No comments:

Post a Comment

HABARI ZILIZOPITA

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...