Leo nimeona nitupie haya maneno niliyoyaimba katika wimbo wangu wa Jina la Yesu, ili na wewe upate kubarikiwa na kuona thamani ya jina la YESU
Rose Muhando
Habari njema kwako kuhusu jina la Yesu,
Rose Muhando
Habari njema kwako kuhusu jina la Yesu,
Raha yangu ni jina la Yesu
Uzima wangu ni jina la Yesu
Habari yangu ni jina la Yesu
Ni jina jema kwa watu wote.
Linasisimua ukilisikia.
Linaleta raha kulitamka.
Linafanya mambo ukiliamini
Jina hilo
waliolikataa, lakini kwa wengine limetujengea heshima.
Jina la Yesu ni kwa wgonjwa, ni afya kwao
Jina la Yesu kwa maskini
Jina la Yesu kwa walioachwa
Jina la Yesu kwa walemavu
Jina la Yesu kwa waliosahauliwa ni tumaini Jipya
Jina la Yesu waliolikataa wasomi limetujenge heshima
Jina la Yesu kwa waimbaji
Jina la Yesu kwa yatima
Jina la Yesu ni uzima kwetu
Jina la Yesu lina thamani
Jina nalipenda sana,
Jina libarikiwe
Jina liheshimiwe na watu wote, Jina linaokoa
Hatukuwa hivi kama
mnavyotuona.
Tulidharauliwa na kukataliwa.
Kwenye jamii yetu tulisahauliwa.
Tulipowauliza swali walitukemea.
Tulipotoa hoja walitudharau.
Lakini Yesu mwenye huruma akayaoona mateso yetu,
akatukumbatia.
Kuna mjina mengi duniani lakini hili ni kiboko.
Jamni mimi nimesikia majina mengi, lakini hili la Yesu ni
mwanzo mwisho.
Nimesikia majina katika viatbu na doria, lakini hili ni
mwanzo mwisho.
Hata kama kwa wengine halifai lakini kwangu limenipandisha
juu hili jina la Yesu.
Jina la Yesu lina herufi chache, lakini linafanya mambo
makubwa.
Acheni nilipende hili jina la Yesu.
MUNGU AKUBARIKI
Mwandishi
Rulea sanga