ROSE MUHANDO HR BANNER

ROSE MUHANDO HR BANNER

ROSE MUHANDO SONG OF THE WEEK

Monday, December 17, 2012

ROSE MUHANDO ANG'ARA TAMASHA LA SHANGWE KAGERA


Mwimbaji nyota wa muziki wa gospel nchini Rose Muhando pamoja na waimbaji wenzake waliweza kulipendezesha tamasha kubwa la Shangwe Kagera zilizofanyika katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na kukusanya mamia ya wakazi wa mji huo pamoja na viongozi wa dini na serikali.

Tamasha hilo liliandaliwa na kampuni ya Beula Communication kwa lengo la kukusanya fedha ili kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu mkoani Kagera. Kati ya viongozi waliohudhuria tamasha hilo ni pamoja na mkuu wa wilaya Bukoba bibi Zippora Pangani, bwana Melkzedek Mutayabarwa ambaye ndiye kiongozi wa kampuni ya Beula iliyoandaa tamasha hilo pamoja na wauguzi kutoka kituo cha watoto cha Tumaini cha mjini humo.

 
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili,Rose Muhando akiimba kwenye Tamasha la shangwe Kagera katika uwanja wa Kaibata mjini Bukoba mwishoni mwa wiki.
Rose Muhando akiimba mbele ya meza kuu katika tamasha hilo.
Mchungaji Edward Mutashobya akisalimiana na Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Rose Muhando wakati wa tamasha la shangwe Kagera katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Baadhi ya watu waliohudhuria tamasha hilo uwanja wa Kaitaba.

Enock Jonas akilishambulia jukwaa katika tamasha hilo, Jonas anatamba na wimbo wema wa Mungu umenizunguka a.k.a shetani na mama mkwe wake wanaliaaa.


Bwana Melkzedek Mutayabarwa akizungumza katika tamasha hilo.
Mkuu wa wilaya ya Bukoba bibi Zippora Pangani akizungumza na mamia ya watu waliohudhuria tamasha hilo.

Waimbaji wa kwaya ya vijana kanisa kuu la  Kilutheri Bukoba mjini wakimsifu Mungu katika tamasha hilo.
Wauguzi kutoka kituo cha Tumaini Children's Centre wakiwa katika tamasha hilo.
Picha kwa hisani ya Africa-yetu.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment

HABARI ZILIZOPITA

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...