ROSE MUHANDO HR BANNER

ROSE MUHANDO HR BANNER

ROSE MUHANDO SONG OF THE WEEK

Saturday, September 12, 2015

ASKOFU MH. DK. GERTRUDE RWAKATARE AMUUNGA MKONO MGOMBEA UDIWANI KATA YA KAWE Mh. MUTTA ROBERT RWAKATARE SIKU YA JUMAMOSI


Mgombe Udiwani Kata ya Kawe jijini Dar es Salaam, Mh. Mutta Robert Rwakatare siku ya leo Jumamosi 12.09.2015 katika viwanja vya Tanganyika Pikers Dar es Salaam aliweza kufungua rasmi kampeni za ugombea Udiwani kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi kata ya Kawe wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam


Kutoka kulia ni Mh. Askofu Dk. Gertrude Rwakatare akiwa na mgombea udiwani Kata ya Kawe Bw. Mutta Robert Rwakatare akiwa amemsika mke wake wakielekea katika viwanja vya Tanganyika Pikers Kawe

Katika kampeni hizi kulikuwa na viongozi mbalimbali kutoka kata mbalimbali waliokuja kumuunga mkono Mh. Mutta Robert Rwakatare. Na hii inatokana na ushirikiano wake mzuri na viongozi walioko madarakani akiwa kama Raoisi wa Mchezo wa ngumi Tanzania.

Mgombe Ubunge Kappi Warioba aliweza kufika katika ufunguzi huu wa kampeni akiwa na Mh. Dk. Gertrude Rwakatare ambaye ni mama mzani wa Mutta Robert Rwakatare. Waheshimiwa hawa waliwaomba wananchi kumchangua Mh. Mutta Gertrude Rwakatare kutokana na utendaji wake mzuri katika ujenzi wa Taifa.

Watu wengi waliweza kujitokeza kumuunga mkono Mh. Mutta R. Rwakatare, na hii ni kutokana na kupendwa na wakazi wa Kata ya Kawe.

Mh. Mutta Gertrude Rwakatare aliweza kuomba wakazi wa Kawe kumpigia kura ili akiingia madarakani aweza kuondooa kero za wakazi wa Kawe kama vile Uhaba wa maji, kulikarabati daraja la Kawe, kuboresha elimu, kuinua michezo na burudani kwa wasanii wa muziki nchini, kuikarabati barabara za Kawe, kutetea haki za hati miliki na mengine mengi

Unaweza kutembelea
www.rumaafrica.blogspot.com kujua mengi kuhusu harakati za Udiwani Kata ya Kawe


Askofu Dk. Gertrude Rwakatare

 Mgombea Ubunge Mh. Kippi Warioba aliyevalia shati la yello akielekea jukwaani
 Mzee Makasii akiimba

BONYEZA "READ MORE" HAPO CHINI KUONA MATUKIO YOTE YA KAMPENI


 No comments:

Post a Comment

HABARI ZILIZOPITA

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...